Ad-Dukhaan 44:14
الدخانثُمَّ تَوَلَّوْا۟ عَنْهُ وَقَالُوا۟ مُعَلَّمٌ مَّجْنُونٌ
Na wao wakamgeuzia uso, na wakasema: 'Huyu amefunzwa, naye ni mwendawazimu.'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wao wakamgeuzia uso, na wakasema: Huyu amefunzwa, naye ni mwendawazimu. [14]
[14] Kisha wakaacha kumsadiki Mtume aliye tiliwa nguvu na miujiza iliyo wazi, na wakamwambia: Huo uwongo na uzushi! Mara nyengine wakimsingizia kuwa amefunzwa hayo na mtu, na mara nyengine kuwa akili yake imekorogeka.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
kisha wakaenda kinyume naye na wakasema kwamba alifundishwa na binadamu au makuhani au mashetani, na kwamba yeye ni mwendawazimu na si Mtume?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net