Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 44 · Aya ya 10

Ad-Dukhaan 44:10

الدخان

فَٱرْتَقِبْ يَوْمَ تَأْتِى ٱلسَّمَآءُ بِدُخَانٍ مُّبِينٍ

Maana

Basi ingoje siku ambayo mbingu zitakapoleta moshi ulio dhahiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi ingoje siku ambayo mbingu zitakapo leta moshi ulio dhaahiri, [10]

[10] Basi ewe Mtume! Ngojea ukame utapo wateremkia, wakasibiwa na kukonda na udhaifu wa kuona, ikawa mtu huwa anaona baina ya mbingu na ardhi moshi dhaahiri shaahiri, akawa anasikia mvumo wake wala hauoni.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi ngojea, ewe Mtume, uwaone hawa washirikina siku ambayo mbingu itakuja na moshi wa wazi

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ad-Dukhaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net