Az-Zukhruf 43:3
الزخرفإِنَّا جَعَلْنَـٰهُ قُرْءَٰنًا عَرَبِيًّا لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ
Hakika Sisi tumeifanya Qur-ani kwa Kiarabu ili mfahamu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika Sisi tumeifanya Qur'ani kwa Kiarabu ili mfahamu. [3]
[3] Hakika Sisi tumeijaalia Qur'ani iwe kwa lugha ya Kiarabu, ili mweze kuelewa umuujiza wake, na mweze kuzingatia maana zake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika sisi tumeiteremsha Qur’ani kwa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), kwa lugha ya Kiarabu, huenda nyinyi mkaelewa na mkazingatia maana yake na hoja zake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net