Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 10

Az-Zukhruf 43:10

الزخرف

ٱلَّذِى جَعَلَ لَكُمُ ٱلْأَرْضَ مَهْدًا وَجَعَلَ لَكُمْ فِيهَا سُبُلًا لَّعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ

Maana

Ambaye amewafanyieni ardhi kama tandiko, na akawafanyieni ndani yake njia mpate kuongoka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ambaye amekufanyieni ardhi kama tandiko, na akakufanyieni ndani yake njia mpate kuongoka. [10]

[10] Ambaye amekufanyieni ardhi ni pahala palipo tanda, ili muweze kukaa humo na mjitumilie, na akakufanyieni ndani yake njia mnazo zipitia katika safari zenu mpate kufikia mtakako.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Aliyewafanyia ardhi kuwa ni (kama) tandiko na mkeka, Akawasahilishia humo njia za maisha yenu na biashara zenu, ili mjiongoze kwa njia hizo kwenye maslahi yenu ya kidini na ya kidunia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net