Ash-Shura 42:53
الشورىصِرَٰطِ ٱللَّهِ ٱلَّذِى لَهُۥ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ ۗ أَلَآ إِلَى ٱللَّهِ تَصِيرُ ٱلْأُمُورُ
Njia ya Mwenyezi Mungu ambaye ni vyake Yeye tu vilivyomo mbinguni na katika ardhi. Jueni kuwa mambo yote yanarudi kwa Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Njia ya Mwenyezi Mungu ambaye ni vyake Yeye tu viliomo mbinguni na katika ardhi. Jueni kuwa mambo yote yanarudi kwa Mwenyezi Mungu. [53]
[53] Njia ya Dini ya Mwenyezi Mungu ambaye ndiyo vyake Yeye tu peke yake, vyote viliomo mbinguni na katika ardhi, kwa kuumba, na kupanga, na kuendesha. Naye ananabihisha, Subhanahu, kwamba kwake Yeye peke yake ndio yanarejea mambo yote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Njia ya Allah Mtukufu Aliye na mamlaka ya vyote vilivyoko mbinguni na vilivyoko ardhini, hana mshirika katika hayo. Jua utambue kwamba kwa Allah Mtukufu, enyi watu, yatarudi mambo yote yenu ya kheri na shari, na huko Amlipe kila mtu kwa matendo yake, yakiwa mema alipwe wema na yakiwa mabaya alipwe ubaya.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net