Ash-Shura 42:51
الشورىوَمَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُكَلِّمَهُ ٱللَّهُ إِلَّا وَحْيًا أَوْ مِن وَرَآئِ حِجَابٍ أَوْ يُرْسِلَ رَسُولًا فَيُوحِىَ بِإِذْنِهِۦ مَا يَشَآءُ ۚ إِنَّهُۥ عَلِىٌّ حَكِيمٌ
Na haikuwa kwa mwanadamu kwamba Mwenyezi Mungu amsemeze ila kwa Wahyi (Ufunuo), au kwa nyuma ya kizuizi, au kumtuma Mjumbe. Naye humfunulia ayatakayo kwa idhini yake. Hakika Yeye ni Mtukufu, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na haikuwa kwa mwanaadamu kwamba Mwenyezi Mungu amsemeze ila kwa Wahyi (Ufunuo), au kwa nyuma ya pazia, au kumtuma Mjumbe. Naye humfunulia ayatakayo kwa idhini yake. Hakika Yeye ni Mtukufu, Mwenye hikima. [51]
[51] Wala haimfalii mtu kusemezwa na Mwenyezi Mungu ila iwe kwa Wahyi (Ufunuo) kwa kumtilia ilhamu katika moyo wake, au usingizini, au kwa kusikia maneno ya Kiungu bila ya kumwona Asemaye, au kwa kutumwa Malaika akaonekana sura yake, na akasikilizana sauti, akamfunulia Nabii kwa idhini ya Mwenyezi Mungu kama atakayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtenda nguvu, basi haziwiliki Mwenye kupita ukomo hikima yake katika kuendesha mambo yake na kupanga kwake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na haipasi kwa kiumbe yoyote, kati ya binadamu, Allah Mtukufu Aseme naye isipokuwa kwa njia ya wahyi ambao Allah Mtukufu Anamtumia, au Aseme naye nyuma ya pazia, kama vile Alivyosema Allah Mtukufu, Aliyetakasika, na Mûsã, amani imshukie, Au Atume mjumbe, kama anavyomtuma Jibrili, amani imshukie, kwa yule anayetumwa kwake ampelekee wahyi wa kile Allah Mtukufu Anataka apelekewe, kwa idhini ya Mola wake, na sio kwa matakwa yake. Hakika Yake Yeye, Aliyetukuka, Yuko juu kwa dhati Yake, majina Yake, sifa Zake na vitendo Vyake. amekishinda kila kitu, na viumbe vyote vimemdhalilikia, ni Mwingi wa hekima katika uedeshaji Wake mambo ya viumbe Vyake. Katika aya hii pana kuthibitisha sifa ya kusema kwa Allah Mtukufu Aliyetukuka, kwa namna inayonasibiana na haiba Yake na ukubwa wa mamlaka Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net