Ash-Shura 42:47
الشورىٱسْتَجِيبُوا۟ لِرَبِّكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِىَ يَوْمٌ لَّا مَرَدَّ لَهُۥ مِنَ ٱللَّهِ ۚ مَا لَكُم مِّن مَّلْجَإٍ يَوْمَئِذٍ وَمَا لَكُم مِّن نَّكِيرٍ
Muitikieni Mola wenu Mlezi kabla haijafika siku isiyoepukika, itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Siku hiyo hamtakuwa na pa kukimbilia wala hamtakuwa na cha kukingia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Muitikieni Mola wenu Mlezi kabla haijafika siku isiyo epukika itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Siku hiyo hamtakuwa pa kukimbilia wala hamtakuwa na cha kukingia. [47]
[47] Enyi watu! Kimbilieni kuitikia aliyo kuitieni Mtume wa Mwenyezi Mungu aliye kuumbeni na akakuleeni, nayo ni Imani na Ut'iifu, kabla uhai haujamaliza fursa ya kutenda vitendo, na ikafika Siku ya Hisabu ambayo Mwenyezi Mungu hairudishi nyuma tena baada ya kwisha ihukumia. Siku hiyo hamtakuwa na pa kukimbilia pa kukuhamini na adhabu, wala hapana cha kuzuia kitakacho kufikieni.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Itikieni mwito wa Mola wenu, enyi wenye kukanusha, kwa kuamini na kutii kabla haijaja Siku ya Kiyama ambayo Haiwezekani kuirudisha. Siku hiyo hamtakuwa na mahali pa kukimbilia penye kuwaokoa na adhabu wala mahali pa kuwasitiri mkawa hamuonekani. Katika aya hii pana dalili ya ubaya wa kuchelewesha, na pana maamrisho ya kuharakisha kufanya kila tendo zuri linalomtokea mja, kwani kuchelewesha kuna athari mbaya na vizuizi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net