Ash-Shura 42:43
الشورىوَلَمَن صَبَرَ وَغَفَرَ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمِنْ عَزْمِ ٱلْأُمُورِ
Na anayekuwa na subira, na akasamehe, hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na anaye subiri, na akasamehe, hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa. [43]
[43] Ninaapa: Bila ya shaka, mwenye kuvumilia kudhulumiwa, akamwachilia aliye mdhulumu, wala asiitetee nafsi yake, pindi ikiwa huko kusamehe kwenyewe hakuupalilii ufisadi ukapata nguvu katika nchi, hakika hayo ni katika mambo ambayo yanatakikana mwenye akili ajilazimishe kuyatenda.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na yoyote mwenye kuvumilia juu ya kero na akalipa, kwa ovu alilofanyiwa, kwa kusamehe, basi hayo ni miongoni mwa mambo makubwa yenye kushukuriwa, na vitendo vyenye kusifiwa ambavyo Allah Mtukufu Ameviamrisha na Ameviwekea thawabu nyingi na sifa nzuri.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net