Ash-Shura 42:19
الشورىٱللَّهُ لَطِيفٌۢ بِعِبَادِهِۦ يَرْزُقُ مَن يَشَآءُ ۖ وَهُوَ ٱلْقَوِىُّ ٱلْعَزِيزُ
Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake. Humruzuku amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu, Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake. Humruzuku ampendaye. Naye ni Mwenye nguvu, Mtukufu. [19]
[19] Mwenyezi Mungu, ni mkuu wa kuwafanyia wema waja wake wote. Huwaruzuku awatakao kama anavyo taka. Naye ni Mwenye kushinda kila kitu, Mwenye nguvu asiye shindika.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu ni Mpole kwa waja Wake, Anamkunjulia riziki Anayemtaka na anampunguzia Anayemtaka, Na Yeye Ndiye Mwenye nguvu, ambaye nguvu zote Anazo, Aliye Mshindi katika kuwatesa wenye kumuasi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net