Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 42 · Aya ya 14

Ash-Shura 42:14

الشورى

وَمَا تَفَرَّقُوٓا۟ إِلَّا مِنۢ بَعْدِ مَا جَآءَهُمُ ٱلْعِلْمُ بَغْيًۢا بَيْنَهُمْ ۚ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ إِلَىٰٓ أَجَلٍ مُّسَمًّى لَّقُضِىَ بَيْنَهُمْ ۚ وَإِنَّ ٱلَّذِينَ أُورِثُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ مِنۢ بَعْدِهِمْ لَفِى شَكٍّ مِّنْهُ مُرِيبٍ

Maana

Na hawakufarikiana ila baada ya kuwajia elimu kwa sababu ya husuda iliyokuwa baina yao. Na lau kuwa haikwisha tangulia kauli kutoka kwa Mola wako Mlezi ya kuahirisha mpaka muda maalumu, basi bila ya shaka pangelihukumiwa baina yao. Na hakika wale waliorithishwa Kitabu baada yao wanakitilia shaka inayowahangaisha.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hawakufarikiana ila baada ya kuwajia ilimu kwa sababu ya husuda iliyo kuwa baina yao. Na lau kuwa haikwisha tangulia kauli kutoka kwa Mola wako Mlezi ya kuakhirisha mpaka muda maalumu, basi bila ya shaka palingeli hukumiwa baina yao. Na hakika walio rithishwa Kitabu baada yao wanakitilia shaka inayo wahangaisha. [14]

[14] Wala hawakukhitalifiana katika Dini wafuasi wa Mitume walio tangulia ila baada ya kuwafikia ujuzi wa kweli, na hayo ni kwa kutokana na uadui na uhasidi ulio baina yao. Na lau kuwa si ahadi iliyo kwisha tangulia kutoka kwa Mwenyezi Mungu ya kuakhirisha adhabu mpaka Siku ya Kiyama, basi bila ya shaka walingeli teketezwa. Na kwa hakika wale walio rithishwa Kitabu kutokana na walio kabla yao, na wakawahi zama zako, wana shaka na Kitabu chao, tena shaka ya kuwatatanisha. Ndio maana hawaitikii wito wako. (Lau kuwa Mayahudi wameamini kweli yaliyomo katika Taurati, wangeli muamini Nabii Isa na Nabii Muhammad. Na lau kuwa Wakristo wameamini kweli yaliomo katika Taurati na Injili basi hapana la kuwazuia wasimuamini Nabii Muhammad, na kumuamini Mwenyezi Mungu Mmoja, wala hana Utatu. Lakini hawana imani ya yakini, na kwa hivyo wameunda mawazo yaliyo nje ya Taurati na nje ya Injili.)

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hawakutengana wenye kumshirikisha Allah Mtukufu katika dini zao wakawa mapote na makundi mbalimbali isipokuwa baada ya ujuzi kuwajia na hoja kuwasimamia. Na hakuna lililowafanya wao wafanye hivyo isipokuwa ni udhalimu na ushindani. Na lau si neno lililotangulia linalotoka kwa Mola wako, ewe Mtume, la kucheleweshwa adhabu mpaka kipindi kilichotajwa. nacho ni Siku ya Kiyama, hukumu ingetolewa ya kuharakishiwa adhabu wakanushaji miongoni mwao. Na hakika wale waliorithishwa (Taurati na Injili), baada ya hawa wenye kutafautiana juu ya haki, wako kwenye shaka yenye kutia kwenye wasiwasi na kutafautiana juu ya Dini na Imani.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shura

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net