Fussilat 41:53
فصلتسَنُرِيهِمْ ءَايَـٰتِنَا فِى ٱلْـَٔافَاقِ وَفِىٓ أَنفُسِهِمْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُ ٱلْحَقُّ ۗ أَوَلَمْ يَكْفِ بِرَبِّكَ أَنَّهُۥ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ شَهِيدٌ
Tutawaonyesha Ishara zetu katika upeo wa mbali na katika nafsi zao wenyewe mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli. Je, haikutoshi kwamba Mola wako Mlezi kuwa Yeye ni Shahidi bora wa kila kitu?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Tutawaonyesha Ishara zetu katika upeo wa mbali na katika nafsi zao wenyewe mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli. Je! Haikutoshi kwamba Mola wako Mlezi kuwa Yeye ni Shahidi wa kila kitu? [53]
[53] Karibuni hivi tutawaonyesha hao wanao zikataa Ishara zetu zenye kuonyesha ukweli wako katika pande za mbinguni na ardhi, na katika nafsi zao wenyewe, mpaka yawadhihirikie ya kwamba uliyo waletea ni Haki tupu si vinginevyo. Je! Wanakataa kuwa Sisi tunawaletea Ishara hizo? Je! Haitoshi kuwa Mola wako Mlezi ni Mwenye kukizunguka kila kitu?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Tutawaonyesha, hawa wakanushaji, aya zetu za kuteka miji na kupata nguvu Uislamu katika maeneo mbalimbali, na juu ya dini nyingine na maeneo ya mbingu na ardhi, na katika matukio makubwa Anayoyaleta Allah Mtukufu humo, na ndani ya nafsi zao, na vile vilivyomo humo miongoni mwa alama za kuvutia za utendakazi wa Allah Mtukufu na maajabu ya utengenezaji Wake, (tutawaonyesha hayo yote) mpaka iwabainikie ubainifu usiokubali shaka yoyote, kwamba Qur’ani ndiyo haki iliyoletwa kwa njia ya wahyi kutoka kwa Mola wa viumbe wote. Je hauwatoshi wao ushahidi wa Allah Mtukufu Aliyetukuka kuwa ni dalili ya kuwa Qur’ani ni haki na kuwa aliyekuja nayo ni mkweli? Kwani Allah Mtukufu Ameishuhudilia kwa kuisadikisha, na Yeye ni shahidi wa kila kitu, na hakuna kitu chochote chenye kutolea ushahidi kuliko ushahidi wa Allah Mtukufu, aliyetakasika na kutukuka.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net