Fussilat 41:42
فصلتلَّا يَأْتِيهِ ٱلْبَـٰطِلُ مِنۢ بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِۦ ۖ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ
Haukifikii upotovu mbele yake wala nyuma yake. Kimeteremshwa na Mwenye hekima, Msifiwa mno.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hautakifikia upotovu mbele yake wala nyuma yake. Kimeteremshwa na Mwenye hikima, Msifiwa. [42]
[42] Hakika wanao ikataa Qur'ani Tukufu inapo wajia bila ya kuzingatia, watapata adhabu ambayo hapana mtu anaye weza kuikadiria. Wao wameipinga Qur'ani nacho hakika ni Kitabu kisicho kuwa na mfano, kinamshinda kila mwenye kukipinga, hakiingiliwi na upotofu usio kuwa na asli kwake kwa upande wowote ule, kimeteremka kwa kukufuatana kutokana na Mungu aliye takasika na upuuzi, Msifiwa kwa wingi wa sifa kwa neema alizo zitoa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ubatilifu haukifikii kutoka upande wowote katika pande Zake, na hakuna kitu chenye kukibatilisha, kwani hiko kimetunzwa kisipunguzwe wala kisizidishwe. Ni teremsho kutoka kwa Mwingi wa hekima katika kuendesha mambo ya waja Wake, Mwenye kushukuriwa kwa sifa za ukamilifu Alizonazo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net