Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 41 · Aya ya 4

Fussilat 41:4

فصلت

بَشِيرًا وَنَذِيرًا فَأَعْرَضَ أَكْثَرُهُمْ فَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ

Maana

Kitoacho habari njema, na chenye kuonya. Lakini wengi katika wao wamepuuza; kwa hivyo hawasikii.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kitoacho khabari njema, na chenye kuonya. Lakini wengi katika wao wamepuuza; kwa hivyo hawasikii. [4]

[4] Chenye kuwapa khabari njema Waumini wenye kutenda kuwa watapata neema iliyo andaliwa kwa ajili yao, na kuwakhofisha wanao kanusha kuwa watapata adhabu chungu iliyo andaliwa kwa ajili yao. Lakini wengi walikitupilia mbali, wala wasinafiike nacho, kama kwamba hawakusikia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hali ya kuwa ni yenye kubashiri malipo ya haraka na ya baadaye kwa anayeiamini na akafanya matendo yanayolingana nayo, na ni yenye kuonya adhabu ya haraka na ya badaye kwa anayeikanusha. Hivyo basi wengi wa watu waliipa mgongo wakawa hawaisikii kusikia kwa kukubali na kuitikia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Fussilat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net