Fussilat 41:19
فصلتوَيَوْمَ يُحْشَرُ أَعْدَآءُ ٱللَّهِ إِلَى ٱلنَّارِ فَهُمْ يُوزَعُونَ
Na siku watakapokusanywa maadui wa Mwenyezi Mungu kwenye Moto, nao wakigawanywa kwa makundi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na siku watakapo kusanywa maadui wa Mwenyezi Mungu kwenye Moto, nao wakikgawanywa kwa makundi. [19]
[19] Ewe Nabii! Siku watakapo kusanywa maadui wa Mwenyezi Mungu kupelekwa Motoni, wakawa wa mwanzo wao wanakutana na wa mwisho wao, ili ipate hoja ilazimike juu ya wote,
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Siku ambayo maadui wa Allah Mtukufu watakusanywa wapelekwe kwenye Moto wa Jahanamu, Malaika wa adhabu watawarudisha wa mwanzo wao wawakusanye na wa mwisho wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net