Al-Ghaafir 40:78
غافروَلَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلًا مِّن قَبْلِكَ مِنْهُم مَّن قَصَصْنَا عَلَيْكَ وَمِنْهُم مَّن لَّمْ نَقْصُصْ عَلَيْكَ ۗ وَمَا كَانَ لِرَسُولٍ أَن يَأْتِىَ بِـَٔايَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ ٱللَّهِ ۚ فَإِذَا جَآءَ أَمْرُ ٱللَّهِ قُضِىَ بِٱلْحَقِّ وَخَسِرَ هُنَالِكَ ٱلْمُبْطِلُونَ
Na bila ya shaka tuliwatuma Mitume kabla yako. Wengine katika hao tumekusimulia habari zao, na wengine hatukukusimulia. Na haiwi Mtume alete Ishara yoyote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Basi ikija amri ya Mwenyezi Mungu, huhukumiwa kwa Haki, na hapo wapotovu watahasiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na bila ya shaka tuliwatuma Mitume kabla yako. Wengine katika hao tumekusimulia khabari zao, na wengine hatukukusimulia. Na haiwi Mtume alete Ishara yoyote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Basi ikija amri ya Mwenyezi Mungu huhukumiwa kwa Haki, na hapo wapotofu watakhasiri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika tuliwatuma kabla yako, ewe Mtume, Mitume wengi kwa watu wao wawalinganie na wavumilie udhia wao. Miongoni mwao kuna wale tuliokuhadithia habari zao, na miongoni mwao kuna wale ambao hatukukuhadithia. Na wote hao wameaminiwa kufikisha wahyi wa Allah Mtukufu kwa watu wao. Na haikuwa ni yenye kuwezekana kwa yoyote miongoni mwao kuleta alama yoyote miongoni mwa alama zinazoonekana au zinazofahamika isipokuwa kwa idhini ya Allah Mtukufu na matakwa Yake. Basi itakapokuja amri ya Allah Mtukufu ya kuadhibiwa wakanushaji, itatolewa hukumu ya uadilifu baina ya Mitume na wale waliowakanusha, na hapo watapata hasara waliokuwa wabatilifu kwa kule kumzulia kwao Allah Mtukufu urongo na kuabudu kwao asiyekuwa Yeye.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net