Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 40 · Aya ya 74

Al-Ghaafir 40:74

غافر

مِن دُونِ ٱللَّهِ ۖ قَالُوا۟ ضَلُّوا۟ عَنَّا بَل لَّمْ نَكُن نَّدْعُوا۟ مِن قَبْلُ شَيْـًٔا ۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ ٱللَّهُ ٱلْكَـٰفِرِينَ

Maana

Badala ya Mwenyezi Mungu? Watasema: Wametupotea, bali tangu zamani hatukuwa tukiomba kitu! Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anawaachia makafiri wapotelee mbali.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Badala ya Mwenyezi Mungu? Watasema: Wametupotea, bali tangu zamani hatukuwa tukiomba kitu! Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anawaachia makafiri wapotelee mbali.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Badala ya Allah Mtukufu? Je watawatetea nyinyi leo? Basi waiteni ili wawaokoe na balaa hili lililowashukia iwapo wataweza. Hapo wakanushaji watasema, «Wametupotea machoni hatuwaoni, na hawakutunufaisha kitu chochote.» Hapo watakubali kuwa wao walikuwa ujingani katika mambo yao, na kuwa kule kuabudu kwao wale waungu kulikuwa ni ubatilifu usio na faida yoyote. Na kama vile Allah Mtukufu Alivyowapoteza hawa waliowapotea katika moto wa Jahanamu waliokuwa wakiwaabudu badala ya Allah Mtukufu, ndivyo Allah Mtukufu Anavyowapoteza wale wenye kumkanusha.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ghaafir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net