Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 40 · Aya ya 67

Al-Ghaafir 40:67

غافر

هُوَ ٱلَّذِى خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ مِنْ عَلَقَةٍ ثُمَّ يُخْرِجُكُمْ طِفْلًا ثُمَّ لِتَبْلُغُوٓا۟ أَشُدَّكُمْ ثُمَّ لِتَكُونُوا۟ شُيُوخًا ۚ وَمِنكُم مَّن يُتَوَفَّىٰ مِن قَبْلُ ۖ وَلِتَبْلُغُوٓا۟ أَجَلًا مُّسَمًّى وَلَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ

Maana

Yeye ndiye aliyewaumba kwa udongo, kisha kwa tone la manii, kisha kwa pande la damu, kisha akawatoa katika hali ya mtoto mchanga, kisha mpate kufikilia utu uzima, kisha mpate kuwa wazee. Na kati yenu wapo wanaokufa kabla, na ili mfikie muda uliokwisha wekwa, na ili mpate kufahamu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Yeye ndiye aliye kuumbeni kwa udongo, kisha kwa tone la manii, kisha kwa pande la damu, kisha akakutoeni katika hali ya mtoto mchanga, kisha mpate kufikilia utu uzima, kisha mpate kuwa wazee. Na kati yenu wapo wanao kufa kabla, na ili mfikie muda ulio kwisha wekwa, na ili mpate kufahamu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Yeye Ndiye Aliyemuumba baba yenu Ᾱdam kwa mchanga, kisha Akawafanya mpatikane kutokana na manii kwa uwezo Wake, na baada yake mnahamia kwenye pande la damu nzito iliyo nyekundu, kisha mnapitiwa na muda kadha ndani ya vizazi, mpaka mnapozaliwa mkiwa watoto wadogo, kisha umbile lenu linapata nguvu (na mnaendelea hivyo) mpaka mnapokuwa wazee, na miongoni mwenu kuna wanaokufa kabla ya hapo. Na ili mfikie kwa miongo hii kipindi kilichotajwa ambacho hapo umri wenu ukome. mzitie akilini hoja za Allah Mtukufu katika hilo na mzizingatie aya zake mjue kuwa hakuna Mola isipokuwa Yeye Anayefanya hilo, na kwamba Yeye Ndiye Ambaye haitakiwi kuabudiwa isipokuwa Yeye.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ghaafir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net