Al-Ghaafir 40:50
غافرقَالُوٓا۟ أَوَلَمْ تَكُ تَأْتِيكُمْ رُسُلُكُم بِٱلْبَيِّنَـٰتِ ۖ قَالُوا۟ بَلَىٰ ۚ قَالُوا۟ فَٱدْعُوا۟ ۗ وَمَا دُعَـٰٓؤُا۟ ٱلْكَـٰفِرِينَ إِلَّا فِى ضَلَـٰلٍ
Nao watasema: Je, hawakuwa wakikufikieni Mitume wenu kwa hoja zilizo wazi? Watasema: Kwani? Watasema: Basi ombeni! Na maombi ya makafiri hayawi ila ni kupotea bure.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Nao watasema: Je! Hawakuwa wakikufikieni Mitume wenu kwa hoja zilio wazi? Watasema: Kwani? Watasema: Basi ombeni! Na maombi ya makafiri hayawi ila ni kupotea bure.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Washika hazina wa Jahanamu waseme kuwaambia kwa njia ya kuwakaripia na kuwalaumu, «Maombi haya hayatafaa kitu. Kwani hawakuwajia nyinyi Mitume wenu na hoja za wazi kutoka kwa Allah Mtukufu na mkawakanusha?» Hapo wale wakanushaji walikubali hilo na waseme, «Ndio, wametujia.» Na washika hazina wa Jahanamu wajiepushe na wao na waseme, «Sisi hatutawaombea wala kuingilia kati kuhusu nyinyi. Ombeni nyinyi wenyewe, lakini dua hiyo haitafaa kitu, kwa kuwa nyinyi ni makafiri, na hayawi maombi ya makafiri isipokuwa ni yenye kupotea, hayakubaliwi wala hayaitikiwi».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net