Al-Ghaafir 40:46
غافرٱلنَّارُ يُعْرَضُونَ عَلَيْهَا غُدُوًّا وَعَشِيًّا ۖ وَيَوْمَ تَقُومُ ٱلسَّاعَةُ أَدْخِلُوٓا۟ ءَالَ فِرْعَوْنَ أَشَدَّ ٱلْعَذَابِ
Wanaonyeshwa Moto asubuhi na jioni. Na itapofika Saa ya Kiyama, patasemwa: Waingizeni watu wa Firauni katika adhabu kali kabisa!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wanaonyeshwa Moto asubuhi na jioni. Na itapo fika Saa ya Kiyama patasemwa: Waingizeni watu wa Firauni katika adhabu kali kabisa!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwanza walipatikana na gharika wakaangamia, kisha wakawa wanaadhibiwa ndani ya makaburi yao ambapo Moto unaletwa kwao, asubuhi na jioni, mpaka wakati wa kuhesabiwa. Na Siku ambayo Kiyama kitasimama kutasemwa, «Watieni Motoni jamaa wa Fir’awn ukiwa ni malipo ya matendo mabaya waliyoyatenda.» Aya hii ndio msingi wa kuthibitisha adhabu ya kaburini.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net