Al-Ghaafir 40:41
غافروَيَـٰقَوْمِ مَا لِىٓ أَدْعُوكُمْ إِلَى ٱلنَّجَوٰةِ وَتَدْعُونَنِىٓ إِلَى ٱلنَّارِ
Na enyi watu wangu! Kwa nini mimi nakuiteni kwenye wokovu, nanyi mnaniita kwenye Moto?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na enyi watu wangu! Kwa nini mimi nakuiteni kwenye uwokofu, nanyi mnaniita kwenye Moto?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na enyi watu wangu! Vipi mimi ninawalingania kumuamini Allah Mtukufu na kumfuata Mtume Wake Mûsã, nao ni ulinganizi utakaowafanya nyinyi muishie Peponi na muwe mbali na vitisho vya Moto, na nyinyi mnanilingania kufanya matendo yenye kupelekea kwenye adhabu ya Allah Mtukufu na mateso Yake Motoni?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net