Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 40 · Aya ya 4

Al-Ghaafir 40:4

غافر

مَا يُجَـٰدِلُ فِىٓ ءَايَـٰتِ ٱللَّهِ إِلَّا ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فَلَا يَغْرُرْكَ تَقَلُّبُهُمْ فِى ٱلْبِلَـٰدِ

Maana

Hawazibishi Ishara za Mwenyezi Mungu ila wale waliokufuru; basi kusikudanganye wewe kutangatanga kwao katika nchi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hawazibishi Ishara za Mwenyezi Mungu ila walio kufuru; basi kusikughuri wewe kutanga tanga kwao katika nchi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakuna anayejadili kuhusu aya za Allah Mtukufu na dalili Zake za kutolea ushahidi umoja wa Allah Mtukufu, akawa anazikabili kwa ubatilifu isipokuwa wapinzani wenye kukataa kuwa Yeye Ndiye Mola wa kweli Anayestahiki kuabudiwa Peke Yake. Basi kusikudanganye wewe kule kutanga kwao mijini katika aina mbalimbali za biashara, shughuli za kuchuma, starehe za ulimwenguni na uzuri wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ghaafir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net