Al-Ghaafir 40:35
غافرٱلَّذِينَ يُجَـٰدِلُونَ فِىٓ ءَايَـٰتِ ٱللَّهِ بِغَيْرِ سُلْطَـٰنٍ أَتَىٰهُمْ ۖ كَبُرَ مَقْتًا عِندَ ٱللَّهِ وَعِندَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ۚ كَذَٰلِكَ يَطْبَعُ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ قَلْبِ مُتَكَبِّرٍ جَبَّارٍ
Hao ambao wanajadiliana katika Ishara za Mwenyezi Mungu pasipo ushahidi wowote uliowafikia, ni chukizo kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya wale walioamini. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu azibavyo kila moyo wa jeuri anayejivuna.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hao ambao wanajadiliana katika Ishara za Mwenyezi Mungu pasipo ushahidi wowote ulio wafikia, ni chukizo kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya walio amini. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu apigavyo muhuri juu ya kila moyo wa jeuri anaye jivuna.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wale wanaobishana na aya za Allah Mtukufu na hoja Zake kwa kuzipinga bila kuwa na hoja zenye kukubalika, upinzani wao huo unawaletea machukivu makubwa kwa Allah Mtukufu na kwa wale walioamini, kama alivyopiga Allah Mtukufu mhuri kwenye nyoyo za hawa wapinzani na akazifunika zisiongoke, ndivyo Anavyoupiga mhuri moyo wa kila mwenye kiburi cha kumfanya akatae kumpwekesha Allah Mtukufu na kumtii, aliye mjeuri sana kwa wingi wa udhalimu wake na uadui wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net