Al-Ghaafir 40:20
غافروَٱللَّهُ يَقْضِى بِٱلْحَقِّ ۖ وَٱلَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِۦ لَا يَقْضُونَ بِشَىْءٍ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْبَصِيرُ
Na Mwenyezi Mungu huhukumu kwa haki; lakini hao ambao wao wanawaomba badala yake hawahukumu chochote. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kuona.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mwenyezi Mungu huhukumu kwa haki; lakini hao wanao waomba badala yake hawahukumu chochote. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia Mwenye kuona.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Allah Mtukufu Anahukumu baina ya watu kwa uadilifu kwa kumpa kila mtu haki yake. Na wale waungu wanaoabudiwa badala ya Allah Mtukufu, hawahukumu chochote kwa kutoweza kwao kufanya hivyo. Hakika Allah Mtukufu Ndiye Mwenye kuyasikia maneno ya waja Wake, Ndiye Mwenye kuyaona matendo wanayoyafanya, na Atawalipa kwayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net