Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 40 · Aya ya 18

Al-Ghaafir 40:18

غافر

وَأَنذِرْهُمْ يَوْمَ ٱلْـَٔازِفَةِ إِذِ ٱلْقُلُوبُ لَدَى ٱلْحَنَاجِرِ كَـٰظِمِينَ ۚ مَا لِلظَّـٰلِمِينَ مِنْ حَمِيمٍ وَلَا شَفِيعٍ يُطَاعُ

Maana

Na waonye siku inayokurubia, wakati nyoyo zitakapofika kooni, nao wamejaa huzuni. Madhalimu hawatakuwa na rafiki, wala mwombezi wa kuitikiwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na waonye siku inayo kurubia, wakati nyoyo zitakapo fika kooni, nao wamejaa huzuni. Madhaalimu hawatakuwa na rafiki, wala mwombezi wa kuitikiwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na uwaonye watu, ewe Mtume, na Siku ya Kiyama iliyo karibu, ingawa wao waiona kuwa iko mbali, pindi nyoyo za waja, kwa kuogopa mateso ya Allah Mtukufu, zitakapopanda juu vifuani mwao na kushikana na koo zao, na hali wao wamejawa na huzuni. Madhalimu hawatakuwa na jamaa wa karibu wala rafiki wala muombezi wa kuwaombea kwa Mola wao akawa ni mwenye kukubaliwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ghaafir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net