Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 40 · Aya ya 16

Al-Ghaafir 40:16

غافر

يَوْمَ هُم بَـٰرِزُونَ ۖ لَا يَخْفَىٰ عَلَى ٱللَّهِ مِنْهُمْ شَىْءٌ ۚ لِّمَنِ ٱلْمُلْكُ ٱلْيَوْمَ ۖ لِلَّهِ ٱلْوَٰحِدِ ٱلْقَهَّارِ

Maana

Siku watakayodhihiri wao. Hapana kitakachofichikana chochote chao kwa Mwenyezi Mungu. Ufalme ni wa nani leo? Ni wa Mwenyezi Mungu, Mmoja, Mshindi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Siku watakayo dhihiri wao. Hapana kitacho fichikana chochote chao kwa Mwenyezi Mungu. Ufalme ni wa nani leo? Ni wa Mwenyezi Mungu Mmoja Mtenda nguvu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Siku ya Kiyama watajitokeza viumbe mbele ya Mola wao, hakuna chochote kuhusu wao au kuhusu matendo yao waliyoyafanya ulimwenguni kitakachofichika kwa Allah Mtukufu. Hapo Atasema Allah Mtukufu Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, «Ni wa nani ufalme na mamlaka Siku ya Leo?» Na Ajijibu Mwenyewe, «Ni vya Allah Mtukufu Aliyepwekeka kwa majina Yake, sifa Zake na vitendo Vyake, Mwenye kutendesha nguvu, Aliyevishinda viumbe vyote kwa uwezo Wake na utukufu wake».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ghaafir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net