Al-Ghaafir 40:12
غافرذَٰلِكُم بِأَنَّهُۥٓ إِذَا دُعِىَ ٱللَّهُ وَحْدَهُۥ كَفَرْتُمْ ۖ وَإِن يُشْرَكْ بِهِۦ تُؤْمِنُوا۟ ۚ فَٱلْحُكْمُ لِلَّهِ ٱلْعَلِىِّ ٱلْكَبِيرِ
Hayo ni hivyo kwa sababu mlikuwa akiombwa Mwenyezi Mungu peke yake mnakataa. Na akishirikishwa mnaamini. Basi hukumu ni ya Mwenyezi Mungu Mtukufu Mkuu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hayo ni hivyo kwa sababu mlikuwa akiombwa Mwenyezi Mungu peke yake mnakataa. Na akishirikishwa mnaamini. Basi hukumu ni ya Mwenyezi Mungu Mtukufu Mkuu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Adhabu hiyo itakayowapata, enyi makafiri, ni kwa sababu ya kuwa nyinyi mlikuwa mkiitwa kwenye kumpwekesha Allah Mtukufu na kumtakasia matendo mema mnalikanusha hilo, na ashirikishwapo Allah Mtukufu mnaliamini hilo na mnalifuata. Basi Allah Mtukufu Ndiye Muamuzi kwa viumbe wake, Ndiye Muadilifu Asiyedhulumu, Anamuongoza Ananayemtaka na Anampoteza Anayemtaka, Anamrehemu Anayemtaka na Anamuadhibu Anayemtaka. Hapana Mola isipokuwa Yeye, Aliye juu kidhati, kicheo na kinguvu (kupitisha Analolitaka).
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net