Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 40 · Aya ya 10

Al-Ghaafir 40:10

غافر

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ يُنَادَوْنَ لَمَقْتُ ٱللَّهِ أَكْبَرُ مِن مَّقْتِكُمْ أَنفُسَكُمْ إِذْ تُدْعَوْنَ إِلَى ٱلْإِيمَـٰنِ فَتَكْفُرُونَ

Maana

Kwa hakika wale waliokufuru watanadiwa: Bila ya shaka kukuchukieni Mwenyezi Mungu ni kukubwa kuliko kujichukia nyinyi nafsi zenu, mlipokuwa mnaitwa kwenye Imani nanyi mnakufuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwa hakika wale walio kufuru watanadiwa: Bila ya shaka kukuchukieni Mwenyezi Mungu ni kukubwa kuliko kujichukia nyinyi nafsi zenu, mlipo kuwa mnaitwa kwenye Imani nanyi mkakataa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika ya wale waliokanusha kuwa Allah Mtukufu Ndiye Mola wa haki na wakaielekeza ibada kwa asiyekuwa Yeye, watakapovishuhudia wenyewe vitisho vya Moto watajichukia machukivu makubwa, na hapo walinzi wa Moto wa Jahanamu watawaita na kuwaambia, «Machukivu ya Allah Mtukufu kwenu huko ulimwenguni, Alipowataka nyinyi mumuamini Yeye na muwafuate Mitume Wake na mkakataa, yalikuwa makubwa zaidi kuliko vile mnavyojichukia nyinyi wenyewe hivi sasa, baada ya kujua kwenu kuwa mnastahili hasira za Allah Mtukufu na adhabu Yake».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ghaafir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net