An-Nisaa 4:168
النساءإِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَظَلَمُوا۟ لَمْ يَكُنِ ٱللَّهُ لِيَغْفِرَ لَهُمْ وَلَا لِيَهْدِيَهُمْ طَرِيقًا
Hakika, wale waliokufuru na wakadhulumu, hakuwa Mwenyezi Mungu ni wa kuwafutia dhambi wala kuwaongoa njia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wale walio kufuru na wakadhulumu hawi Mwenyezi Mungu kuwasamehe wala kuwaongoa njia. [168]
[168] Wale walio kufuru, na wakajidhulumu nafsi zao, na wakamdhulumu Mtume kwa kuupinga ujumbe wake, na wakawadhulumu watu walipo wafichia Haki, Mwenyezi Mungu hatowasamehe kamwe maadamu watabaki katika ukafiri wao. Wala hatawapa uwongofu wa kuijua njia ya kuvuka. Sio mtindo wake Subhanahu kuwasamehe watu kama hao nao wangali kubaki katika upotovu wao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika wale waliomkanusha Allah Mtukufu na Mtume Wake na wakadhulumu kwa kuendelea kwao na ukafiri, Allah Mtukufu Hatakuwa ni Mwenye kuwasamehe madhambi yao wala kuwaongoza njia ya kuwaokoa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net