An-Nisaa 4:166
النساءلَّـٰكِنِ ٱللَّهُ يَشْهَدُ بِمَآ أَنزَلَ إِلَيْكَ ۖ أَنزَلَهُۥ بِعِلْمِهِۦ ۖ وَٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ يَشْهَدُونَ ۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدًا
Lakini Mwenyezi Mungu anayashuhudia yale aliyokuteremshia wewe. Aliyateremsha kwa elimu yake, na Malaika pia wanashuhudia. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi wa sawasawa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Lakini Mwenyezi Mungu anayashuhudia aliyo kuteremshia wewe. Ameyateremsha kwa kujua kwake - na Malaika pia wanashuhudia. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi. [166]
[166] Lakini ikiwa hao watu hawashuhudii kukusadikisha, basi Mwenyezi Mungu Mwenyewe anashuhudia kuwa aliyo kuteremshia ni sahihi. Hakika Yeye amekuteremshia hayo kwa hikima, na kwa mujibu wa ujuzi wake. Na Malaika nao wanashuhudia hayo kadhaalika. Na ewe Mtume! Yakutosha wewe ushahidi wa Mwenyezi Mungu, kuliko ushahidi wowote mwenginewe.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Iwapo Mayahudi na wengineo watakukanusha, ewe Mtume, hakika Allah Mtukufu Anashuhudia kuwa wewe ni Mtume Wake Aliyemteremshia Qur’ani tukufu; Ameiteremsha kwa ujuzi Wake. Na vilevile Malaika wanashuhudia ukweli wa wahyi uliyoletewa. Na ushahidi wa Allah Mtukufu Peke Yake unatosha.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net