Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 39 · Aya ya 72

Az-Zumar 39:72

الزمر

قِيلَ ٱدْخُلُوٓا۟ أَبْوَٰبَ جَهَنَّمَ خَـٰلِدِينَ فِيهَا ۖ فَبِئْسَ مَثْوَى ٱلْمُتَكَبِّرِينَ

Maana

Itasemwa: Ingieni milango ya Jahannamu mdumu humo. Basi nayo ni ubaya ulioje wa makazi ya wanaotakabari!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Itasemwa: Ingieni milango ya Jahannamu mdumu humo. Basi nayo ni ubaya ulioje wa makaazi ya wanao takabari! [72]

[72] Wataambiwa: Iingieni milango ya Jahannamu mliyo jaaliwa mkae humo milele. Jahannamu ni pahala paovu mno pa kukaa wenye kutakabari na wakakataa kuikubali Haki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wataambiwa wale wenye kukataa kuwa Allah Mtukufu Ndiye Mola wa haki, kwa kuwatweza na kuwadhalilisha, «Ingieni kwenye milango ya Jahanamu, hali ya kukaa humo milele.» Ni mbaya mno mwisho wa wale wanaolifanyia kiburi jambo la kumuamini Allah Mtukufu na kufuata kivitendo sheria Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zumar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net