Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 39 · Aya ya 43

Az-Zumar 39:43

الزمر

أَمِ ٱتَّخَذُوا۟ مِن دُونِ ٱللَّهِ شُفَعَآءَ ۚ قُلْ أَوَلَوْ كَانُوا۟ لَا يَمْلِكُونَ شَيْـًٔا وَلَا يَعْقِلُونَ

Maana

Au ndio wanachukua waombezi badala ya Mwenyezi Mungu? Sema: Ingawa hawana mamlaka juu ya kitu chochote, wala hawatambui lolote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Au ndio wanachukua waombezi badala ya Mwenyezi Mungu? Sema: Ingawa hawana mamlaka juu ya kitu chochote, wala hawatambui lolote? [43]

[43] Bali washirikina wakawafanya wengineo badala ya Mwenyezi Mungu kuwa ni waombezi wao wa kuwakurubisha kwake. Waambie, ewe Muhammad: Mnafanya haya ijapo kuwa hawa mnao wafanya "waombezi" hawanacho wanacho kimiliki, wala hawana wanacho kifahamu?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Au kwani hawa wanaomshirikisha Allah Mtukufu wamewachukua badala Yake Yeye waungu wao wanaowaabudu wakawafanya ni waombezi wakuwaombea kwa Allah Mtukufu katika haja zao? Waambie, «Je mnawafanya ni waombezi kama mnavyodai, ingawa waungu hao hawamiliki chochote na hawafahamu kamwe kuwa nyinyi mnawaabudu?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zumar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net