Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 39 · Aya ya 3

Az-Zumar 39:3

الزمر

أَلَا لِلَّهِ ٱلدِّينُ ٱلْخَالِصُ ۚ وَٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُوا۟ مِن دُونِهِۦٓ أَوْلِيَآءَ مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَآ إِلَى ٱللَّهِ زُلْفَىٰٓ إِنَّ ٱللَّهَ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ فِى مَا هُمْ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهْدِى مَنْ هُوَ كَـٰذِبٌ كَفَّارٌ

Maana

Hakika Dini Safi ni ya Mwenyezi Mungu tu. Na wale wanaowafanya wenginewe kuwa ni walinzi wakisema: Sisi hatuwaabudu ila wapate kutujongeza tu kumkaribia Mwenyezi Mungu - Hakika Mwenyezi Mungu atahukumu baina yao katika wanayohitalifiana. Hakika Mwenyezi Mungu hamwongoi aliye mwongo kafiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika Dini Safi ni ya Mwenyezi Mungu tu. Na wale wanao wafanya wenginewe kuwa ni walinzi wakisema: Sisi hatuwaabudu ila wapate kutujongeza tu kumkaribia Mwenyezi Mungu - Hakika Mwenyezi Mungu atahukumu baina yao katika wanayo khitalifiana. Hakika Mwenyezi Mungu hamwongoi aliye mwongo kafiri. [3]

[3] Jueni na mtambue kwamba Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye Dini isiyo kuwa na ila. Na washirikina walio wafanya wenginewe kuwa ni wasaidizi wa kuwanusuru, wanasema: Sisi hatuwaabudu hawa kwa kuwa ni waumbaji, bali tunawaabudu wapate kutukaribisha kwa Mwenyezi Mungu, kwa mkaribisho wa kutuombea sisi kwake Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu atahukumu baina ya hawa washirikina na Waumini wenye kumuabudu Mwenyezi Mungu Mmoja katika yale wanayo khitalifiana katika matatizo ya shirki na Tawhidi. Hakika Mwenyezi Mungu hamjaalii afikie Haki mtu ambaye mtindo wake ni uwongo na kukanya.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Jua utanabahi kwamba ni haki ya Allah Mtukufu, Peke Yake, kutiiwa utiifu uliyotimia uliosalimika na ushirikina. Na wale wanaomshirikisha mwingine pamoja na Allah Mtukufu wakawafanya wasiokuwa Yeye kuwa ni wategemewa, wanasema, «Hatuwaabudu waungu hawa pamoja na Allah Mtukufu isipokuwa wapate kutuombea kwa Allah Mtukufu na ili watukurubishe daraja Kwake.» Hivyo basi wakakufuru, kwani ibada na uombezi ni wa Allah Mtukufu, Peke Yake. Hakika Allah Mtukufu atawatenganisha, Siku ya Kiyama, baina ya Waumini wenye ikhlasi na wale wenye kumshirikisha mwingine pamoja na Allah Mtukufu, katika yale waliokuwa wanatafautiana juu yake kuhusu vile walivyoabudu. Hapo amlipe kila mmoja kwa anachostahiki. Hakika Allah Mtukufu hawaelekezi kuongoka kwenye njia iliyonyooka wale wenye kumzulia urongo Allah Mtukufu, wenye kuzikanusha aya Zake na hoja Zake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zumar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net