Saad 38:88
صوَلَتَعْلَمُنَّ نَبَأَهُۥ بَعْدَ حِينٍۭ
Na bila ya shaka mtajua habari zake baada ya muda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na bila ya shaka mtajua khabari zake baada ya muda. [88]
[88] Na hapana shaka nyinyi, mnao ikadhibisha Qur'ani, mtakuja jua karibuni hivi ukweli uliomo ndani yake wa ahadi, na maonyo, na khabari za mambo yatakayo kuja, na Ishara za ulimwengu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na mtajua, tena mtajua, enyi washirikina, habari ya hii Qur’ani na ukweli wake, pindi utakaposhinda Uislamu na watu kuingia kwenye dini ya Allah Mtukufu mapote kwa mapote, na pia pindi mtakaposhukiwa na adhabu na kamba zote kuwakatikia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net