Saad 38:72
صفَإِذَا سَوَّيْتُهُۥ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِن رُّوحِى فَقَعُوا۟ لَهُۥ سَـٰجِدِينَ
Na nitakapomkamilisha na kumpulizia roho inayotokana nami, basi muangukieni kwa kumtii.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na nitakapo mkamilisha na kumpulizia roho inayo tokana nami, basi muangukieni kwa kumt'ii. [72]
[72] Nikisha timiza kumuumba na nikampulizia siri ya uhai, nayo ni roho, muangukieni kwa kusujudu sijida ya kumtukuza na kumuamkia.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi nitakapousawazisha mwili wake na umbo lake na nikapuliza roho ndani yake na uhai ukatambaa humo, msujudieni sijida ya heshima na kukirimu, na siyo sijida ya ibada na kutukuza. Kwani ibada haiwi isipokuwa kwa Allah Mtukufu, Peke Yake. Na Allah Mtukufu Ameharamisha, katika Sheria ya Kiislamu, kusujudu kwa njia ya maamkizi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net