Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 38 · Aya ya 35

Saad 38:35

ص

قَالَ رَبِّ ٱغْفِرْ لِى وَهَبْ لِى مُلْكًا لَّا يَنۢبَغِى لِأَحَدٍ مِّنۢ بَعْدِىٓ ۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلْوَهَّابُ

Maana

Akasema: Mola wangu Mlezi! Nisamehe na unipe ufalme usiomwelekea yeyote baada yangu. Hakika Wewe ndiye Mpaji.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema: Mola wangu Mlezi! Nisamehe na unipe ufalme usio mwelekea yeyote baada yangu. Hakika Wewe ndiye Mpaji. [35]

[35] Suleiman alimwomba Mola wake Mlezi kwa kurejea kwake: Mola wangu Mlezi! Nighufirie yaliyo toka kwangu kwa ghafla, na unitunukie ufalme usio elekea yeyote kuupata baada yangu. Hakika Wewe ndiye Mwingi wa kutunukia, na ndiye Mwingi wa kutoa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na akasema, «Mola wangu! Nisamehe dhambi zangu na unipe ufalme mkubwa unaohusika na mimi ambao mfano wake hautakuwa kwa binadamu yoyote baada yangu. Hakika yako wewe, Uliyetakasika na kutukuka, ni Mwingi wa upaji na utoaji».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saad

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net