Saad 38:33
صرُدُّوهَا عَلَىَّ ۖ فَطَفِقَ مَسْحًۢا بِٱلسُّوقِ وَٱلْأَعْنَاقِ
(Akasema:) Nirudishieni hao! Basi akaanza kuwapapasa miguu na shingo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Nirudishieni! Akaanza kuwapapasa miguu na shingo. [33]
[33] Akaamrisha warudishwe tena kwake apate kujua hali yao. Akaingia kuwapapasa miundi ya miguu yao na shingo zao kwa upole na mapenzi juu yao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Warudisheni hao farasi walioorodheshwa hivi punde. Wakarudishwa, na akaingia kuipiga miguu yao na shingo zao kwa upanga kwa kujikurubisha kwa Allah Mtukufu, kwa kuwa wao walikuwa ni sababu ya Swala yake kumpita, Na ilikuwa kujikurubisha kwa Allah Mtukufu kwa kuchinja farasi inakubaliwa katika Sheria yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net