Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 38 · Aya ya 31

Saad 38:31

ص

إِذْ عُرِضَ عَلَيْهِ بِٱلْعَشِىِّ ٱلصَّـٰفِنَـٰتُ ٱلْجِيَادُ

Maana

Alipopelekewa jioni farasi wasimamao kidete, tayari kutoka shoti.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Alipo pelekewa jioni farasi wasimamao kidete, tayari kutoka shoti; [31]

[31] Na hebu taja katika khabari za Suleiman kuwa alipelekewa alasiri farasi wa asli ambao hutulia wanapo simama, na huenda mbio wanapo kwenda.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kumbuka pindi walipoorodheshwa mbele yake kipindi cha alasiri farasi wa asili wenye kasi za kukimbia, waliosimama kwa miguu mitatu na kuinua mguu wa nne kwa kuwa ni farasi bora na wapesi. Waliendelea kuorodheshwa mbele yake mpaka jua likachwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saad

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net