Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 38 · Aya ya 24

Saad 38:24

ص

قَالَ لَقَدْ ظَلَمَكَ بِسُؤَالِ نَعْجَتِكَ إِلَىٰ نِعَاجِهِۦ ۖ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ ٱلْخُلَطَآءِ لَيَبْغِى بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ وَقَلِيلٌ مَّا هُمْ ۗ وَظَنَّ دَاوُۥدُ أَنَّمَا فَتَنَّـٰهُ فَٱسْتَغْفَرَ رَبَّهُۥ وَخَرَّ رَاكِعًا وَأَنَابَ ۩

Maana

Akasema: Kweli amekudhulumu kwa kumtaka kondoo wako mmoja kuongezea kwenye kondoo wake. Na hakika washirika wengi hudhulumiana wao kwa wao, isipokuwa walioamini na wakatenda mema. Na hao ni wachache. Na Daudi akajua kuwa tumemfanyia mtihani. Basi akamwomba msamaha Mola wake Mlezi, na akaanguka kusujudu na kutubia.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema: Kweli amekudhulumu kwa kumtaka kondoo wako mmoja kuongezea kwenye kondoo wake. Na hakika washirika wengi hudhulumiana wao kwa wao, isipo kuwa walio amini na wakatenda mema. Na hao ni wachache. Na Daudi akajua kuwa tumemfanyia mtihani. Basi akamwomba msamaha Mola wake Mlezi, na akaanguka kusujudu na kutubia. [24]

[24] Daudi akasema kabla hajasikia maneno ya yule mwenye ugomvi mwengine: Hakika huyo amekudhulumu kwa kumtaka kondoo wako amchanganye na wale wake. Na hakika wengi wenye kushirikiana hudhulumiana wao kwa wao, isipo kuwa wale ambao Imani yao imetulia katika nyoyo zao, na wakawa wanatenda mema. Na watu kama hao ni wachache, shida kupatikana. Na Daudi akajua kuwa jambo hili si chochote ila ni mtihani tuliyo mfanyia Sisi. Basi akaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu, na akainama kurukuu kwa Mwenyezi Mungu, na akarejea kwa Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Dãwûd akasema, «Kwa hakika ndugu yako amekudhulumu kwa kutaka kwake kumchukua kondoo wako awe pamoja na kondoo wake. Na kwa hakika, wengi wa washirika, baadhi yao wanadhulumu wengine: wanawadhulumu kwa kuchukua haki zao na kukosa kuwa waadilifu wa nafsi zao. Isipokuwa watu wema walioamini, kwani wao hawadhulumiani, nao ni wachache.» Na Dãwûd akajua kwa yakini kuwa sisi tumemtahini kwa ugomvi huu, hivyo basi akamuomba msamaha Mola wake, akasujudu kwa kujikurubisha kwa Allah Mtukufu na akarejea Kwake na akatubia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saad

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net