Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 38 · Aya ya 21

Saad 38:21

ص

وَهَلْ أَتَىٰكَ نَبَؤُا۟ ٱلْخَصْمِ إِذْ تَسَوَّرُوا۟ ٱلْمِحْرَابَ

Maana

Na je, imekufikia habari ya wagombanao walipopindukia ukuta kuingia chumbani?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na je! Imekufikia khabari ya wagombanao walipo pindukia ukuta kuingia chumbani? [21]

[21] Ewe Muhammad! Ati imekujia khabari ya makhasimu wagombanao, walio mjia Daudi kwa kupindukia kuta za mihrabuni palipo kuwa pahala pake pa ibada? Hawakupita mlangoni.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na je, ilikujia, ewe Mtume, habari ya wagomvi wawili waliovuka ukuta wakamuingilia Dãwûd mahali pake pa kuabudu?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saad

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net