Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 38 · Aya ya 19

Saad 38:19

ص

وَٱلطَّيْرَ مَحْشُورَةً ۖ كُلٌّ لَّهُۥٓ أَوَّابٌ

Maana

Na pia ndege waliokusanywa makundi kwa makundi; wote walikuwa wanyenyekevu kwake.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na pia ndege walio kusanywa makundi kwa makundi; wote walikuwa wanyenyekevu kwake. [19]

[19] Na pia tukamdhalilishia ndege walio kusanywa kutokana na kila namna na kila pahali. Vyote hivyo, milima na ndege, vikimwitikia Daudi kama atakavyo, akivisarifu kama apendavyo kwa maslaha ya umma.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tukawadhalilisha ndege pamoja naye, kwa mkusanyiko wao, wakawa wanasabbih kwa kusabbih yeye na kuwa watiifu kwake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saad

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net