Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 38 · Aya ya 13

Saad 38:13

ص

وَثَمُودُ وَقَوْمُ لُوطٍ وَأَصْحَـٰبُ لْـَٔيْكَةِ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلْأَحْزَابُ

Maana

Na Thamud na kaumu Luti na watu wa Machakani. Hayo ndiyo makundi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Thamud na kaumu Lut'i na watu wa Machakani. Hayo ndiyo makundi. [13]

[13] Na kina Thamudi na Kaumu Lut'i na Kaumu ya Shuaibu, na watu wa Machakani, kwenye miti mingi iliyo shikamana. Hao ndio walio jumuika kuwapinga Mitume wao kama walivyo jumuika watu wako.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Thamûd, watu wa Lûṭ, watu wa miti na mabustani, nao ni watu wa Shu‛ayb. Hao ndio ummah walioshirikiana wakawa pote moja juu ya ukafiri na ukanushaji na wakajikusanya juu yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saad

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net