As-Saaffaat 37:91
الصافاتفَرَاغَ إِلَىٰٓ ءَالِهَتِهِمْ فَقَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ
Basi akaiendea miungu yao kwa siri, akaiambia: Mbona hamli?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi akaiendea miungu yao kwa siri, akaiambia: Mbona hamli? [91]
[91] Akayaendea kwa haraka yale masanamu kwa kificho, na akayapa chakula ambacho wale washirikina walikiweka mbele yao ili nao wapate baraka yao kwa mujibu wa madai yao. Akasema kwa maskhara na kejeli: Mbona hamli?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Akatembea kwa haraka kuelekea kwenye masanamu ya watu wake, akasema kwa njia ya kuwakejeli, «Si mkile chakula hiki ambacho washika mlango wenu wanawapatia?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net