As-Saaffaat 37:87
الصافاتفَمَا ظَنُّكُم بِرَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
Mnamdhania nini Mola Mlezi wa walimwengu wote?"
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mnamdhania nini Mola Mlezi wa walimwengu wote? [87]
[87] Mnamdhania nini huyo ambaye ndiye Mwenye haki ya kuabudiwa kwa kuwa Yeye ndiye Muumba walimwengu wote, mtapo kutana naye na hali nyinyi mmemfanyia washirika wenginewe katika ibada?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mnamdhani Mola wa viumbe vyote Atawafanya nini mkimshirikisha Yeye na mkamuabudu asiyekuwa Yeye?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net