Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 37 · Aya ya 8

As-Saaffaat 37:8

الصافات

لَّا يَسَّمَّعُونَ إِلَى ٱلْمَلَإِ ٱلْأَعْلَىٰ وَيُقْذَفُونَ مِن كُلِّ جَانِبٍ

Maana

Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa huko kila upande.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa huko kila upande. [8]

[8] Hao majabari wa kishetani hawawezi kusikiliza yanayo pita katika ulimwengu wa Malaika. Na wao hupopolewa kwa kila kinacho faa cha kuwazuia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hawawezi hao Mashetani kufika kwenye viumbe vya juu, navyo ni mbingu na Malaika waliyomo ndani yake, wakapata kuwasikiliza wanapoutamka wahyi ambao Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Anauleta, unaokusanya sheria Yake na makadirio Yake, na wanarushiwa vimondo kila upande.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

As-Saaffaat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net