Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 37 · Aya ya 75

As-Saaffaat 37:75

الصافات

وَلَقَدْ نَادَىٰنَا نُوحٌ فَلَنِعْمَ ٱلْمُجِيبُونَ

Maana

Na hakika Nuhu alituita, na Sisi ni bora wa waitikiaji.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hakika Nuhu alitwita, na Sisi ni bora wa waitikiaji. [75]

[75] Na hakika Nuhu alitwita alipo kwisha kata tamaa na watu wake, basi na Sisi tukawa ni wabora wa kuitikia wito wake, tulipo muitikia ombi lake, na tukawaangamiza watu wake kwa tofani.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kwa hakika Alituita kwa kutuomba Nabii wetu Nûḥ tumlinde na watu wake, basi bora wa wenye kumuitikia tulikuwa ni sisi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

As-Saaffaat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net