As-Saaffaat 37:65
الصافاتطَلْعُهَا كَأَنَّهُۥ رُءُوسُ ٱلشَّيَـٰطِينِ
Mashada ya matunda yake kama kwamba ni vichwa vya mashetani.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mashada ya matunda yake kama kwamba vichwa vya mashet'ani. [65]
[65] Matunda yake mabaya kuyatazama, yana sura ya kukirihisha, macho hayapendi kuyatazama, kama vichwa vya mashetani ambavyo kwa hakika watu hawajaviona, lakini mtu humpitikia tu katika dhana jinsi ya ubaya wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Matunda yake yana Sura mbaya sana kama vichwa vya Mashetani.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net