Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 37 · Aya ya 62

As-Saaffaat 37:62

الصافات

أَذَٰلِكَ خَيْرٌ نُّزُلًا أَمْ شَجَرَةُ ٱلزَّقُّومِ

Maana

Je, kukaribishwa hivi si ndiyo bora, au mti wa Zaqqum?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Kukaribishwa hivi si ndio bora, au mti wa Zaqqum? [62]

[62] Je! Hiyo riziki maalumu iliyo andaliwa kwa sababu ya watu wa Peponi ni bora, au mti wa Zaqqum ulio andaliwa kwa ajili ya watu wa Motoni?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, hayo yaliyotangulia kuelezwa ya starehe za Pepo ni makaribisho bora na zawadi kutoka kwa Allah Mtukufu, au ni mti mbaya uliolaaniwa wa zaqqūm, ambao ni chakula cha watu wa Motoni?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

As-Saaffaat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net