Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 37 · Aya ya 53

As-Saaffaat 37:53

الصافات

أَءِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَـٰمًا أَءِنَّا لَمَدِينُونَ

Maana

Ati tukishakufa tukawa udongo na mafupa, ndiyo tutalipwa na kufanyiwa hesabu?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ati tukisha kufa tukawa udongo na mafupa, ndio tutalipwa na kuhisabiwa? [53]

[53] Ati baada ya kwisha teketea, tukawa udongo na mafupa, tutakuja kuwa hai mara nyengine, tuhisabiwe na tulipwe kwa vitendo tulivyo kwisha vitenda?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, tunapokufa, tukakatika vipande vipande na tukawa mchanga na mifupa, kwani ni wenye kufufuliwa, kuhesabiwa na kulipwa kwa matendo yetu?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

As-Saaffaat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net