As-Saaffaat 37:34
الصافاتإِنَّا كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِٱلْمُجْرِمِينَ
Hivyo ndivyo tutakavyowafanyia wahalifu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hivyo ndivyo tutakavyo wafanyia wakosefu. [34]
[34] Hakika mfano wa adhabu hiyo Sisi tunawapa wale walio fanya makosa katika Haki ya Mwenyezi Mungu kwa ushirikina na kutenda maasi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hivi ndivyo sisi tunavyowafanyia waliochagua mambo ya kumuasi Allah Mtukufu ulimwenguni na wakaacha kumtii, basi tutawaonjesha adhabu kali.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net