As-Saaffaat 37:32
الصافاتفَأَغْوَيْنَـٰكُمْ إِنَّا كُنَّا غَـٰوِينَ
Tulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Tulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu. [32]
[32] Tukakuiteni kwenye maasi na upotovu na nyinyi mkaitikia wito wetu. Kazi yetu ni kufanya hila ya kuwaita watu wafuate upotovu tulio nao. Basi hatuna lawama.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ndipo tukawapoteza na njia ya Allah Mtukufu na ya kumuamini, kwa kuwa sisi wenyewe tulikuwa ni wapotevu kabla yenu. Na kwa hivyo tukapotea kwa sababu ya ukafiri wetu na tukawaangamiza nyinyi pamoja na sisi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net